Afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara ametoa ahadi kwa kwa msemaji wa Azam FC Jaffar Idd kuwa wekundu hao watatoka na ushindi katika uwanja wa Chamanzi.
Akizungumza jana walipokutana katika kipindi cha Wednesday Night kinachowakilishwa na mtangazaji wa Azam Tv Patrick Nyembela alimuakikishia msemaji huyo kuwa Simba itaondoka na pointi katika uwanja wa Chamanzi Complex.
"Namtaka Jaffar Idd tupinge naweka ahadi kuwa nitavua kofia yangu nikifungwa na yeye atatoa kizibao chake." Alisema Manara.
Manara ana imani kuwa kitendo cha timu hiyo kuwaacha wachezaji wake sita muhimu ni jambo ambalo litawagharimu Azam mbele ya Simba ambayo imesheheni wachezaji hao ambao mikataba yao ilimalizika.
Simba iliwasajili wachezaji watatu ambao waliachwa na Azam baada ya kumaliza mikataba yao akiwemo Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, John Bocco na Aishi Manula.
Kwa mara ya kwanza Azam na Simba zitacheza mchezo ligi kuu Vodacom katika uwanja wa Chamanzi jijini Dar es Salaam baada ya TFF kupokea kilio cha Azam ambayo kwa muda mrefu aliwataka Simba na Yanga kutumia uwanja wa Chamanzi Complex endapo atakuwa mwenyeji.

Comments
Post a Comment