Timu ya West Ham United maarufu kama wagonga nyundo wa London huenda wakamwondoa meneja wao Slaven Bilic na kumrejesha Roberto Mancin katika ligi ya England kwa mara nyingine.
West Ham hawana furaha na Bilic kutokana na matokeo mabovu wanayopata uwanjani tangu kuanza kwa ligi kuu England na tayari wamepoteza michezo mitatu katika mechi tatu walizocheza mpaka sasa.
West ilipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Manchester United baada ya kufungwa mabao 4-0 katika uwanja wa Old Trafford, ilipoteza dhidi ya Southampton baada ya kufungwa 3-2 katika uwanja wa Olympic na pia dhidi ya Newcastle baada ya kupigwa bao 3-0.
Mancin ambaye kwa sasa ni kocha wa Zenit ya Urusi ni chaguo namba mbili la West Ham baada ya meneja wa Newcastle Rafael Benitez ambaye anaelezwa kukosa furaha kwa waajili wake wa sasa.
Inaelezwa kuwa Benitez ambaye pia aliwahi kuwa kocha wa Liverpool alinyimwa kiasi cha pesa kwa ajili ya kusajili nyota awatakao ili kuleta ushindani ligi kuu.
Mancin amewahi kuwa kocha wa Manchester wa Manchester city na kuipatia timu taji la ubingwa wa ligi kuu kabla ya nafasi yake kuchuliwa na Manuel Pellegrin ambaye alipeleka pia ubingwa kwa timu hiyo.

Comments
Post a Comment