Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amesema kuwa timu yao haina hofu kukabiliana na Azam FC katika uwanja wa Chamanzi.
Mayanja alisema kuwa mchezo huo ni kipimo tosha kwa klabu ya Simba ambayo italazimika kucheza mpira bila kutegemea nguvu kubwa ya mashabiki.
Akizugumzia pia kuhusiana na mabadiliko ya ratiba amesema wanayaheshimu mabadiliko yaliyofanywa na bodi ya ligi kwa kuwa haitaathiri mipango yao.
"Tunaheshimu maamuzi ya bodi ya ligi, Simba haina hofu kucheza kokote pale, iwe Uhuru au Taifa na sehemu nyingine yoyote sisi tumejipanga vizuri alisema." Alisema Mayanja.
Kwa upande wake Mayanja amesisitiza kuwa mabadiliko hayo yatimarisha zaidi kikosi hicho kwa kuwa wachezaji watacheza kwa nguvu na kujituma kama iwavyo mikoani ambapo sapoti ya mashabiki huwa ndogo.
Bodi ya ligi imefanya mabadiliko hapo jana na tayari ratiba inaonesha Simba na Yanga zitamfuata Azam katika uwanja wa Chamanzi Complex msimu huu.

Comments
Post a Comment