Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF limefanya mabadiliko ya muda wa kuanza kwa mchezo wa Azam na Simba hapo kesho katika uwanja wa Chamanzi.
Kwa mujibu wa ratiba ya awali mchezo huo ulitakiwa kuchezwa majira ya saa moja za usiku siku ya kesho.
TFF imefikia uamuzi huo baada ya kupokea ushauri kutoka kwa kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam chini ya mwenyekiti wake Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda.

Comments
Post a Comment