Messi apiga Hat-trick ya kwanza La liga msimu huu.


Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi tayari amefungua ukurasa mpya La liga msimu baada kufunga hat-trick katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Espanyol hapo jana.

Messi alifunga bao hizo katika dakika ya 26, 35 na 67, Gerald Pique aliyefunga bao la nne na Luis Suarez aliyefunga bao la 5 baada ya kupokea pasi safi kutoka Ousmane Dembele ambaye ametua hivi karibuni.

Pia Barcelona iliwatumia nyota wake wapya ambao wamesajiliwa na timu hiyo msimu huu akiwemo kiungo Paulinho pamoja na Ousmane Dembele ambaye ameanza kwa kutengeneza bao la Luis Suarez.

Comments