Baada ya kutamba kwa MSN (Messi, Neymar na Suarez) ambayo inafahamika kama moja ya safu kali ya ushambulizi kuwahi kutokea duniani hatimaye Paris Saint Germain ya Ufaransa imekuja na hii ya CMN.
Ukiizungumzia PSG kwa sasa unainzungumzia CMN ambayo inaundwa na Cavani, Mbappe na Neymar ambayo kwa pamoja waliifungia timu hiyo mabao 4 dhidi ya Metz wikiendi hii.
Katika mechi hiyo Cavani alifunga mabao 2, Kylan Mbappe aliyetoka Monaco na Neymar walifunga bao 1 kila mmoja.
Kocha wa PSG Emery Unai anaamini kuwa timu yake haingalii zaidi ubingwa wa league 1 bali wamejikita zaidi kutamba katika ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa kuwa wana uhakika na matokeo ya nyumbani.
Usajili wa Neymar kwenda PSG imevunja safu ya MSN Barcelona ambayo ilifunga zaidi ya mabao 100.

Comments
Post a Comment