Mashabiki wa Simba wazidi kutamba na usajili wa Okwi.


Ikiwa ni siku moja tangu kumalizika kwa mchezo wa kimataifa wa kufuzu kwenye michuano ya kombe la dunia kati ya Uganda na Misri mashabiki wa Simba wameonesha kuguswa na ubora wa mshambuliaji Emanuel Okwi.

Okwi ambaye alifungua kitabu cha mabao 4 ligi kuu ya Vodacom alifunga bao la ushindi dhidi ya Misri katika dakika ya 52.

Bao pekee la Emanuel Okwi linaifanya Uganda kuongoza kwenye kundi E kwa pointi 7 juu ya Misri yenye pointi 6, Ghana 1 na Congo ambayo haijapata pointi.

Mashabiki wa Simba nchini Tanzania wamekuwa wenye na wameonekana kujivunia tukio hilo linalodhihirisha ubora wa strika.

Eskaone ilifanya utafiti katika mitaa mbali mbali na hali ya nguvu ya ushabiki kwa mashabiki wa Simba imezidi kuwa kubwa hasa baada ya Okwi kuinyanyua Uganda.

"Ni jambo lisilofichika kuwa Okwi ni mchezaji bora ambaye ameiufaisha Simba kwa wakati wote, ni jambo ambalo kwa sasa tunajivunia hata kama anaitwa Mzee." Alisema mmoja wa mashabiki wa Simba.

Baada ya tukio hilo Simba itakuwa na kibarua kizito cha kupambana na Azam katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa siku ya jumatano ya wiki ijayo.

Comments