Kiungo Mshambuliaji wa kimataifa wa Croatia Ivan Perisic huenda akawa amezima rasmi ndoto za kutua Old Trafford baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka 5 Inter Milan.
Perisic mwenye miaka 28 alikuwa akiwindwa kwa udi na uvumba na Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ambaye aliweka mezani ofa ya £44 milioni.
Inter Milan ilionekana kuweka ngumu kwenye makubaliano ya usajili baada ya kudai kiasi cha £48 milioni bado na winga mwenye kasi Antonio Martial.
Hata hivyo Mourinho aliamua kuachana na usajili wa nyota huyo ambaye ameifungia Inter Milan mabao 21 tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Wolfsburg ya Ujermani mwaka 2015.

Comments
Post a Comment