Kiungo mshambuliaji wa Liverpool Phelipe Coutinho ameonesha kuwa mwenye furaha kwenye viwanja wa vya mazoezi huko Mel Wood tofauti na ilivyodhaniwa.
Coutinho ambaye alikuwa akiitumika Brazil imefuzu kuwania tiketi ya kufuzu kwenye kombe la dunia alirudi jana kupitia ndege binafsi na baadhi ya wachezaji wenzake.
Mchezaji huyo alionekana kutaniana na beki wa kushoto wa Liverpool Alberto Moreno muda mfupi baada ya kuwasili Mel Wood.
Pia Coutinho alifanya mazoezi na kikosi cha kwanza ambacho kipo kwenye maandalizi ya kuchuana na Manchester City katika mchezo wa ligi utakaopigwa jumamosi kwenye uwanja wa Etihad.



Comments
Post a Comment