sajili 5 zilizoanza kufanya balaa England.


Mohamed Salah (Liverpool)

Bila kila mfuatiliaji wa mpira ameanza kuona makali ya Mohamed Salah ambaye ameongeza nguvu ya mashambulizi katika kikosi cha Liverpool. Alijiunga na Liverpool akitokea Stoke City kwa ada ya Pauni 39 milioni. Tayari ameshaifungia Liverpool mabao 2 na kutengeneza pasi za mabao.

Alexandre Lacazzete (Arsenal) 

Ni mshambuliaji mpya aliyetua Arsenal akitokea Olympic Lyon ya Ufaransa. Ameanza kudhihirisha kuwa yeye ni bora hata katika ligi ya England ambayo ina ushindani wa hali ya juu. Tayari Lacazzete ameifungia Arsenal mabao 2 katika mechi 4 alizoichezea timu hiyo mpaka sasa na pia ametoa pasi moja ya goli.

Choup Moting (Stoke city)


Ni mshambuliaji mpya aliyesajiliwa na Stoke city akitokea Schakle 04 baada ya kumaliza mkataba wake na wajermani. Moting amezaliwa amezaliwa na kulelewa Ujermani licha ya kuwa kiasili ni Mjermani. Mshambuliaji huyo ameifungia Stoke city mabao mawili katika mchezo wa jana ambapo timu hiyo ilitoka sare ya mabao 2-2 na Man Utd.

Alvaro Morata (Chelsea)

Hakuna ubishi juu ya ubora wa Morata mwenye miaka 24, tangu alipokuwa Real Madrid, Juventus na kurejea Bernabeu kwa mara nyingine. Amejiunga na chelsea kwa ada ya Pauni 70 milioni. Raia huyo wa Hispania Tayari ameanza kuonesha makali yake baada ya kuifungia timu hiyo mabao 3, katika mechi 4 alizocheza.

Romelu Lukaku (Man Utd)

Alijiunga na Manchester United katika dirisha la usajili ambalo lilifungwa hivi karibuni akitokea Everton. Lukaku ameanza kuonesha thamani yake ya pauni 90 milioni ambao mashetani hao wekundu waliitoa kumng'oa Lukaku kutoka Goodson. Tayari ameifungia Man Utd mabao 4.




Comments