Hatimaye kilio cha udhamini kimeanza kusika nchini baada ya Majimaji FC kulamba mkataba wenye thamani ya shilingi milioni 150 kutoka SOKABET.
Majimaji imesaini mkataba wa mwaka mmoja na kampuni hiyo ambayo ilitambulishwa rasmi nchini mwezi Agosti mwaka huu.
Kwa mujibu wa mwakilishi wa SOKABET Franco Ruhinda udhamini huo wa Majimaji uliambatana rasmi na uzinduzi wa huduma za kampuni hiyo.
Kwa upande wa Majimaji kupitia mwenyekiti wao Steven Ngonyani alisema kuwa udhamini huo utaongeza morali na kuongeza nguvu kwenye kikosi chao na kuahidi kuutendea haki.
Majimaji imekuwa klabu ya 9 kupokea udhamini mnono baada zikiwa zimepita siku chache tangu Ndanda FC na Mbao zitangaze kupata mdhamini.

Comments
Post a Comment