Stoke city imekuwa ya kwanza kwenda sawa na kasi ya Manchester United ambayo ilianza nayo msimu huu baada ya kulazimisha sare ya bao 2-2 na timu hiyo.
Usajili mpya wa Stoke city Choupo Moting ndiye aliyetikisa mara mbili nyavu za Manchester United na mabao ya Manchester yaliwekwa nyavuni na Marcus Rashford pamoja na Romelu Lukaku.
Manchester United ilishinda michezo mitatu mfululizo ya ligi kuu baada ya kupata ushindi dhidi ya West Ham, Swansea na Leicester city.
Wababe hao wamefungana pointi 10 na mahasimu wao Manchester City ambayo ilipata ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Manchester City.

Comments
Post a Comment