Washambuliaji wa Yanga Amis Tambwe na Obrey Chirwa hawatasafiri na kikosi cha timu hiyo kuelekea katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Njombe Mji.
Tambwe na Chirwa wameanza mazoezi mapesi chini ya uangalizi wa daktari katika uwanja wa Uhuru lakini imeonakana kuwa hawakuwa tayari kwa kusafiri na timu.
Kocha wa Yanga George Lwandamina amewatoa rasmi wachezaji hao kwenye programu yake katika mchezo dhidi ya Njombe mji utakaopigwa katika uwanja wa Saba saba mkoani hapo.
Mbali na washambuliaji hao pia golikipa Beno Kakolanya, Geoffrey Mwashiuya na Hussein Seif tayari wameanza mazoezi mepesi lakini hawataweza kuungana na kikosi hicho.
Yanga ipo mbioni kusaka ushindi wake wa kwanza baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Lipuli ya Iringa.

Comments
Post a Comment