TFF yamaliza utata, Simba na Yanga kuifuata Azam Chamanzi.


Baada ya kupigwa chenga za hapa na pale kwa muda mrefu hatimaye TFF imeridhia ombi la Azam FC ambayo itakuwa na haki ya kutumia uwanja wake dhidi ya Simba na Yanga.

Kwa muda mrefu Azam imekuwa ikipigania kutumia dimba la chamanzi Complex dhidi ya watani hao wa jadi lakini hata hivyo kwa kigezo cha ufinyu wa majukwaa ulimpeleka Azam katika uwanja wa Taifa.

Kwa mujibu wa TFF kupitia msemaji wake Alfred Lucas alisema kuwa uwanja utaingiza idadi ya watu itakayotosha kiasi kinachokadiriwa jumla ya watu 7000 kwa wataokaa na ulinzi utaimarishwa kuzuia waliokosa.

Uamuzi huo umepokelewa vibaya vibaya na mashabiki wa vilabu vya Simba na Yanga ambao wamedai kuwa idadi ya mashabiki wanaohudhuria uwanjani ni kubwa kulinganishwa na kudai uwanja wa chamanzi hauwezi kukidhi mahitaji.

Azam na Simba zitacheza mchezo huo siku ya jumamosi majira ya saa 1 usiku ili kupisha mchezo wa mapema kati ya Majimaji na Prisons.

Comments