Viingilio Azam vs Simba vyatajwa.


Kuelekea mechi ya Azam na Simba siku ya jumamosi tayari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetaja bei za viingilio za mchezo huo wa ligi kuu Vodacom.

Viingilio vitakuwa ni shilingi 10000 kwa jukwaa la V.I.P wakati kwenye jukwaa la mzunguko ambalo lina uwezo kupokea jumla ya watu 6000, bei yake ni shilingi 7000.

Kwa mara ya kwanza Azam na Simba zinakutana katika uwanja wa Chamanzi Complex baada ya TFF kupokea kilio cha ramba ramba hao ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakiitafuta haki ya kucheza katika uwanja huo.

Kwa mujibu wa TFF kunako msimu huu na kuendelea Simba Yanga zitatakiwa kucheza katika uwanja wa Chamanzi endapo Azam na Simba zitakuwa wageni badala ya kutumia uwanja wa Uhuru au ule wa Taifa kama ilivyozoeleka.

Comments