1. Oxlade Chamberlain (Liverpool)
Ni miongoni mwa wachezaji waliosajili muda mchache kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili akitokea Arsenal na kutua Liverpool.
Chamberlain alikuwa kwenye kikosi cha England ambacho kilipata ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Slovakia hapo jana, hajaonekana kwenye akiitumikia timu yake mpya ambayo itasafiri jijini Manchester katika mchezo wa wikiendi dhidi ya Manchester city. Macho na matarajio ya wengi ni kumuona namba ambavyo winga huyo mwenye kasi atakavyotimiza majukumu yake uwanjani.
2. Mamadou Sakho (C. Palace)
Beki huyo amerejea Crystal Palace alipokuwa kwa mkopo msimu uliopita, amekuwa kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo kutokana na kiwango kikubwa alichokionesha chini ya kocha aliyekuwepo Sam Allardyce.
Baada ya kuondoka rasmi Liverpool hatimaye anaanza maisha mapya chini ya kocha wa sasa Frank De Boer ambaye ni raia wa uholanzi, wachambuzi wengi wamekuwa wakidai kuwa huenda Sakho hatafiti kutokana na aina ya mtindo wa uchezaji ambao unatumiwa na kocha huyo. Kiu ya mashabiki ni kushuhudia akiendelea na ubora ule bado haijaichezea Palace, macho yetu wikiendi hii.
3. Wilfrey Bony (Swansea)
Hatimaye Bony amerejea Swansea kwa mara nyingine baada ya kuchemsha Manchester ambapo alifunga mabao 6 tu. Pia alichemsha Stoke city ambako alipelekwa kwa mkopo. Raia huyo wa Ivory anakumbukwa kutokana na makali yake ya kutupia bao nyavuni alipokuwa Swansea ambapo aliweza kuifungia timu hiyo mabao 26 katika mechi 54. Kiu ya wengi ni kutaka kuona kama Bony atarejea kwenye kiwango chake kama ilivyokuwa hapo awali alivyokuwa na timu hiyo.
4. Renato Sanchez (Swansea)
Akiwa na umri wa miaka 19 anabaki kuwa moja ya viungo wazuri ambao wanapatikana duniani kwa sasa, amejiunga na Swansea kwa mkopo akitokea Bayern Munich. Ukaribu wa kocha Paul Clement na Carlo Ancelloti ambao walifanya kazi pamoja muda mrefu umeiwezesha Swansea kumnasa mchezaji. Kiungo ya wengi ni kutaka kushuhudia Sanchez atakuja ni nguvu gani England, kiungo ni moja kati ya viungo wenye nguvu, kasi na ujuzi wa hali ya juu.
5. Serge Aurier (Tottenham)
Anakamilisha orodha yetu kwa leo, ametua Tottenham kwa dau la £23 milioni, ni beki wa kulia mwenye kasi na kiwango cha hali ya juu. Manchester City ilimpiga bei Kyle Walker kwenda Man city, na imebaki na Kieran Trippier pekee. Macho ya ulimwengu kushuhudia uwezo wa beki huyo kulinganishwa na ule wa Kyle Walker.





Comments
Post a Comment