Meneja Arsene Wenger amesema kuwa Arsenal inaweza kuwa bingwa msimu huu licha ya kuanza vibaya kwenye ligi kuu na kufanya vibaya kwenye soko la usajili.
Arsenal wanacheza na FC Bournemouth leo wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza michezo miwili ya ligi kuu dhidi ya Liverpool na Stoke city.
Kwa upande wa usajili klabu hiyo ilichemsha kumleta Emirates Kylian Mbappe ambaye amejiunga na PSG kwa pamoja na kiungo mshambuliaji Thomas Lemar ambaye ameendelea kubaki Monaco.
Lakini pamoja na yote kocha wa huyo ambaye hajapata ubingwa huo tangu mwaka 2004 haoni sababu kwa nini Arsenal isiwepo kwenye kinyang'anyiro cha Ubingwa msimu huu.
"kwa nini tusiweze? Tumepoteza michezo miwili na yote uugenini bado kuna nafasi ya kujipanga na kuimarika ili kuwa sawa zaidi hapo mbeleni.
"Kikosi chetu kina nguvu, msimu uliopita tulifanikiwa kunyakua pointi 75 na kombe la FA nadhani msimu tuna nafasi ya kufanya vizuri zaidi." Alisema Wenger.
Pia timu hiyo itakuwa na kibarua cha kuchuana na FC Cologne ya Ujermani katika michuano ya Europa Alhamisi ijayo pia itasafiri kuifuta Chelsea katika uwanja wa Stamford Bridge kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu.

Comments
Post a Comment