Yanga kuirudishia Simba fedha za Buswita.


Kamati ya hadhi na haki ya wachezaji imetangaza kuafiki makubaliano yaliyofikiwa baina ya Simba na Yanga ya kumfungulia mchezaji Pius Buswita ambaye alisaini mkataba na klabu zote mbili.

Mchezaji huyo alisaini mkataba wa awali na klabu ya Simba na kupokea kiasi cha shilingi milioni 10 na baadae alisaini Yanga kitendo ambacho ni kinyume na kanuni za usajili kwa mchezaji mmoja kusaini kwenye vilabu mbili tofauti.

kamati hiyo imekubali kumfungulia mchezaji huyo kuitumikia Simba za kwa sharti la kuirudishia Simba kiasi cha shilingi milioni 10 ambazo Buswita alichukua pamoja na kurejesha malipo ya gharama ya tiketi ya ndege ambayo Simba waligharamia.


Comments