Leo tarehe 25, Desemba, jamii ya wakristo ulimwenguni wanasherehekea sherehe za sikukuu ya Christmas. Blog hii ilitembea mtaani ambapo iliweza kukutana na watu kadhaa ambao waliweza kutoa salamu zao za Xmas na mwaka mpya kwa watu mbali mbali....
Tropia Haule, Mbezi makabe.
Anawatakia heri ya Xmas na mwaka familia yake, ndugu na marafiki wote wa karibu, anawataka watanzania kusherekea kwa amani siku ya kuzaliwa kwa Kristo.
Mary Lwambano, Pwani.
Anawakia heri ya Xmas na mwaka mpya familia yake wakiwemo baba, mama, dada na kaka Zake wote. Ujumbe (amewataka wapendane wote).
Semeni, Mbezi Msakuzi.
Semeni a.k.a mama Mustapha anawatakia watanzania wote heri ya sikukuu ya Xmas na mwaka mpya.
Ujumbe: Mwenyezi Mungu atulinde na kutupa amani watanzania.
Godfrey Shayo, Mbezi makabe.
Anawatakia heri ya Xmas na mwaka mpya wakazi wote wa Mbezi makabe. Amewataka watanzia wote wazingatie kufanya kazi.
Wellingtony Fredy, Dar es Salam.
Amewataka heri ya Xmas watanzania wote, amewataka wasiache imani yao kwa Mungu.






Comments
Post a Comment