Inside The Bible: Usikubali wakujue, wakikufahamu inatosha



"Hezekia akawafurahia, akawaonyesha nyumba yake yenye vitu vyake vya thamani, fedha na dhahabu na manukato na marhamu ya thamani, na nyumba yote yenye silaha zake za vita, au vitu vyote vilivyoonekana katika hazina zake; hapakuwa na kitu nyumbani mwake wala katika ufalme wake asichowaonyesha." Isaya 39:2

Ukiendelea hapo katika hiyo sura ya 39 utaona namna nabii Isaya alipeleka ujumbe wa Mungu kwa Hezekia ya kwamba siku za mbele ufalme wa Babeli utachukua vyote alivyowaonyesha.

Kamwe usikubali wakujue, wala wajue mbinu zako, waache wakufahamu tu, mtu akikujua ni rahisi sana kushambulia udhaifu wako na kukushinda, ni rahisi sana kwake kutumia mapungufu yako ili kumweka yeye juu na wewe uanguke

Kwa miaka mia moja tangu miaka ya 1750 hadi 1860 yaani (Karne 1) Taifa la Uingereza halikuwa na mpinzani katika uzalishaji, wao ndiyo walianzisha mapinduzi ya viwanda duniani, walikuwaTaifa lenye nguvu sana kama mwanae na koloni lake la zamani Marekani, leo (USA).

Kwa miaka ile ilikuwa ngumu mno kushindana na England, kwa utajiri, uchumi, biashara hata teknolojia hakuna taifa lilikuwa linafikia hata robo ya uzalishaji wake

Mwaka 1862 Waingereza walifanya maenesho makubwa ya kimataifa yaliyojulikana kama "London Great Exhibition". Yalianza Mei 1 hadi Novemba 15 ya mwaka huo, ni muda usiopungua miezi 5. Wakiwa vipofu wa maandiko 😃 walisahau aliyopitia Hezekia, na waliamua kujimwambafai kupitia ubora wao. Hawakujua majasusi walijaa kila mahala tena wale wa Copy and Paste.

Baada ya tukio lile dunia ilianza kumchalenji Uingereza. Mataifa Kama Ujermani, USA, Ufaransa, Uholanzi yalianza kuja juu na taratibu alipoteza legacy yake (alama) mbele ya Marekani mpaka leo.

Jifunze kwamba:

Pale Mungu anapokubariki wasaidie wengine kwa akili, wapo wengine wenye tamaa ya mafanikio kushinda wewe na pengine hawahitaji nafasi mbili kuusoma udhaifu wako

Kula vizuri, vaa vizuri na waheshimu wengine, sehemu za vikao na ndugu, mikusanyiko ya sherehe au msiba, au kwenye mabaa siyo sehemu ya kutaja kiwango cha mshahara wako au utajiri unaomiliki benki, wapo wenye nia ovu wanaweza kukufanyia hila ukapoteza kila ulichonacho.

Hakuhitaji tabia za kihaya (joke/utani), kuwathibitishia watu mafanikio yako. Watakuona tu aina za gari, vitega uchumi na shule ambazo watoto wanasoma watafahamu tu upo vizuri.

Utajiri wako, na mbinu zako za mafanikio ni Siri yako. Hukatazwi kuwafunza wengine na kuwa msaada kwao lakini wamegee kwa akili ingawa katika ubongo wako unafahamu mahali pa kuwapiga bao wapinzani wako.

Yote kwa yote waruhusu watu wakufahamu, ishi nao vizuri, cheka nao lakini uwe na mipaka vinginevyo utakutana na hatma ya Hezekia. Ipo siku Elon Mask atakwambia kufa na umaskini ni dhambi kwa dunia ya leo ambayo unaweza kupata ujuzi na maarifa hata ukiwa umelala kitandani. Lakini hawezi kukwambia alitajirika namna gani.

Imeandaliwa;
Student wa Bible Class
Kapinga Jr

Comments

Post a Comment