Watu sahihi
👉🏽 Ingawa kila mwanadamu ana thamani, lakini ni jambo jema sana kuchagua watu sahihi wa kuambatana nao.
👉🏽 Daudi alipojificha huko Siklagi watu mashujaa walimfata kuambatana nae. Walikuwa hodari katika upinde, wengine upanga, wengine mkuki na ngao.
👉🏽 Daudi alichagua watu wenye kumsaidia kusonga mbele na siyo kurudi nyuma. Maisha yetu yanahitaji tuambatane na watu sahihi ili tuweze kusonga mbele.
👉🏽 Daudi anajiwa na baadhi ya watu wa kabila la Benjamini na Yuda, anahoji kama wamekuja kwa wema au usaliti (1 Nyakati 12:16-17). Daudi alikuwa sahihi, mtu asiyeendana na mipango yako usiruhusu kuambatana nae
Watu sahihi ni wakina nani? 🤔
1 Mambo ya Nyakati 12:32
Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.
👉🏽 Watu 👆🏽 wenye kuzijua nyakati na yale yatupasayo kufanya kwa muda na wakati sahihi ndiyo marafiki sahihi kwetu. Watu wenye sifa za mfano wa kabila la Isakari ni
> Ni wajuzi wa kuchungulia fursa
> Ni washauri wazuri wa mambo ya biashara na mipango tulio nayo
> Wana jicho la kuona mbali. Wana mipango miaka 10 mbele
> Ni wazuri kwenye kutengeneza bajeti
> Huiona pesa mahali usipoiona pesa
👉🏽 Tunahitaji hawa watu
Jack Ma amewahi kusema, jaribu kutafuta watu sahihi na siyo walio bora.
Unahitaji kuwa mfanya biashara mzuri tafuta watu sahihi wa kuambatana nao, wa kupokea ushauri kwao pia.
Unahitaji wokovu, tafuta sahihi watakaokusaidia kukua katika wokovu, hapa watu wa bata na wazinzi watakufelisha
Maandiko yanasema chuma hunoa chuma, chuma hakionolewi na mbao.
Mithali 27:17
Imendaliwa na
Student wa Bible Class
Kapinga Jr
.jpeg)
Mna mafundisho mema sana.
ReplyDeleteBarikiwa mno mtumishi
Delete