Leo tujifunze kwa kamanda wa Mfalme Daudi, Yoabu mwana wa Seruya
1 Mambo ya Nyakati 11:6
Naye Daudi akasema, Mtu yeyote atakayekuwa wa kwanza wa kuwapiga Wayebusi, yeye atakuwa mkuu na jemadari. Naye wa kwanza aliyepanda ni Yoabu mwana wa Seruya, naye akawa mkuu.
👉🏽 Alikuwa na mapungufu na tamaa lakini Yoabu anabaki kuwa kioo cha watu jasiri na wenye uthubutu wa mambo katika maisha. Hakukubali kuwa mfupi katika mafanikio.
Kwanini Yoabu ni kioo
👉🏽 Hakukubali kuwa wa mwisho, alichagua kuwa wa kwanza. Wapo watu hawafanikiwa kwa sababu hujiona wao ni wa kushindwa tuu, hupenda kuwa mwisho, hawana uthubutu, ni WAFUPI katika uthubutu, maamuzi na kujitoa. Neno la Bwana linasema atatufanya vichwa wala si mikia (Kum 28:13). Unakubali vipi kuwa mkia?
👉🏽 Licha ya kuwa ndugu wa Daudi, hakutaka favor ili kupata cheo, wala upendeleo. Aliingia front kupambana. Kuna watu wengi leo wakiwa na ndugu wenye mali, uwezo na fedha nyingi hubweteka. Yoabu alijua nafasi yake vema. Kwamba mtegemea cha ndugu hufa maskini. Kwamba hakuna kitu rahisi duniani..ni lazma upambane kuinua maisha yako.
Kuna wakati tunahitaji kujiamini kwanza kama tunaweza, Mungu huweka hatua zake kukanyaga na wale ambao wapo tayari kukanyaga kwanza na si kulala kitandani au kushinda kijiweni. Soma habari ya wakoma wanne (2 Wafalme 7:3-14).jpeg)
Comments
Post a Comment