SIRI ZA BIBLIA: Pokea Elimu ya mafanikio kwa huyu jamaa


πŸ‘‰πŸ½ Nakiri kwamba Yabesi amenifanya nipende kufanya maombi, na kufunga kwa bidii. Huyu kwangu ni roli modo. Nampenda mno huyu jamaa wa Yuda. 

πŸ‘‰πŸ½ Akamwomba Bwana mambo MANNE


1. Lau kama ungenibariki kweli kweli 


πŸ‘‰πŸ½Kubali ukatae baraka πŸ‘†πŸ½ndiyo msingi wa kwanza wa mwanadamu. Tunahitaji kubarikiwa ili tustawi Yakobo, Yusufu ni mfano wa hili 


2. Na kunizidishia hozi yangu 


πŸ‘‰πŸ½ Kamwe usimpe Mungu πŸ‘†πŸ½ mipaka, mwache akuinue kwa kadiri apendavyo 


3. Na mkono wako ungekuwa pamoja nami.


πŸ‘‰πŸ½Tunahitaji πŸ‘†πŸ½nguvu za Mungu, hakika tunahitaji ulinzi wake, apigane na wale watakao kupigana nasi, maana vita ni ya Bwana 


4. Nawe ukanilinda dhidi ya uovu usiwe kwa huzuni yangu 


πŸ‘‰πŸ½ Huwezi kubarikiwa πŸ‘†πŸ½kamwe ikiwa dhambi inakuzonga, Yabesi haikutaka dhambi, kwa maana dhambi inaleta huzuni, simanzi na majuto. Ni mzigo wa laana wenye kuleta kikwazo cha kufanikiwa kwenye maisha yetu.


πŸ‘‰πŸ½ Aliomba vizuri naye Bwana akamjibu, akamjalia hayo aliyomwomba.


Kwanini Yabesi alifanikiwa? πŸ‘‡πŸΎ


Mambo ya Nyakati 4:9-10


Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nilimzaa kwa huzuni.


πŸ‘‰πŸ½ Jibu ni rahisi sana. "Heshima", aliyekuwa si mkaidi wala jeuri huenda hata torati ya Bwana aliizingatia, kwa kuwa hakutawaliwa na kiburi. Alijaa unyenyekevu na adabu 


πŸ‘‰πŸ½ Hatuwezi kufanikiwa ikiwa hatumuheshimu Mungu, wazazi, maaskofu na mapadri hata viongozi wa kanisa. Anyway Mungu atusaidie. πŸ‘‡πŸΎ


Maandiko yanasema..."heri wenye moyo safi maana hao watamwona Mungu (Mathayo 5:8) 


πŸ‘‰πŸ½ Ilimchukua miaka mingapi huyu Yabesi kufanikiwa. Sisi hatujui wala maandiko hayasemi, pengine miaka 10 au zaidi ya hapo. Hakuna jambo rahisi, hata kwa Yabesi haikuwa rahisi pia. Tuwe wavumilivu na wenye subira tukiendelea kungoja neema nyingi za Bwana wetu. 

> Vijana wengi huwa tunaamini sana katika mafanikio ya haraka

> Kuna wakati tunahitaji kufanikiwa ikiwa tumemweka Mungu mbali na maisha yetu. Matendo yetu haya hayamvutii 

> Tunawaza kufanikiwa ili tuishi maisha ya Anasa na starehe 

> Tunakata tamaa mapema na kuamini katika milango ya Shortcut,  hatuna subira na uvumilivu

> Tumetawaliwa na uvivu kuanzia akilini na mwilini. Mafanikio yanahitaji kujituma na kufanya kazi kwa bidii bila kuchoka


πŸ‘‰πŸ½ Ikiwa Bwana alimuumba Adamu na kumpa Eden ailime (mwanzo 2:15). Hakutaka akae bure. Msingi wa mwanadamu ni kazi. Maana hata Nuhu alianza kilimo baada ya gharika (mwanzo 9:20). 


πŸ‘‰πŸ½ Ikiwa tunaendelea kuomba na kungojea baraka zake tupambane πŸ˜„, hakuna free lunch duniani.

Comments