👉🏽 Anakwenda mfalme Yeoashi, kuomba mkono wa Bwana kwa nabii wake Elisha, anayemalizia siku zake za mwisho duniani kwa ugonjwa uliomwua.
👉🏽 Elisha akamwambia atwae uta wa mshale na alifungue dirisha upande wa mashariki, Shamu. Napenda maneno ya Elisha 👇🏾
"Akasema, mshale wa Bwana wa kushinda, naam, mshale wa kushinda Shamu...." (2 falme 13:17)
👉🏽 Kwa jina la Bwana milele Sisi ni washindi, na wote wanaotaka kusimama mbele yetu watawekwa nyuma. Kwa kuwa jina la Bwana wa majeshi linaweza yote.
👉🏽 Elisha akamwelekeza mfalme, kupiga chini mishale kama ishara ya kuishinda Shamu. Anakasirishwa kwa kuwa mfalme anapiga mara tatu. Ndipo Elisha akamwambia alitakiwa kupiga zaidi na ndipo angeimaliza kabisa Shamu.
👉🏽 Wakristo wengi wa leo hatuwezi kuimaliza shamu kwa sababu sisi ni wavivu kama mfalme Yeoashi. Hatupendi maombi, hatupendi neno, hatuna muda wa kufunga, hatuweki muda wa kusema na Mungu wetu, ndiyo maana tunashindwa kuwekwa huru kwa kuwa hatuna juhudi na bidii katika maombi. Tu wafupi mno kwa kwa mambo hayo.
Tazama:
👉🏽 Kanisa la kwanza lilikesha na kuomba kwa juhudi na ndipo Mungu alipojibu, ndiyo maana Petro aliachiwa huru mahali alipofungwa 👇🏾
Matendo 12:5
"Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake."
👉🏽 Maandiko yanatuhimiza, tuombe bila kukoma (1 Thesa 5:17), na tuombe kila siku bila kuchoka (Luka 18:1) na ndipo tutakuwa huru. Na siyo kupiga mara tatu kama mfalme Yeoashi, hatutakuwa huru.
Ikiwa twataka kufanikiwa basi kuanzia sasa, tupambanie tulicho nacho kwa bidii bila kuchoka
> Kama ni masomo, soma kwa bidii hadi ufikie ushindi wako
> Kama ni kilimo, lima kwa bidii usichoke
> Ulianzisha kampuni, pambana hadi ufanikiwe kuisimamisha kampuni, usiwezi kijana mwenye kuanzisha na kuacha
> Kama ni biashara maneno ya watu yasikuvunje moto pambana hadi isimame
> Ikiwa ni ndoa pambania wala usichoke
Shetani huwapenda mno walio wavivu, wenye kukata tamaa upesi na wale waliokosa maamuzi. Nehemia aliyajua haya ndiyo maana hakumpa shetani nafasi, hakuacha mavunjiko kwenye ukuta aliojenga.
.jpeg)
Comments
Post a Comment