Hekima ya Mhubiri
Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maafa, wala hekima uko kuzimu uendako wewe." Mhubiri 9:10
Natamani uonapo neno hili la Mhubiri aliyejazwa hekima uamke kitandani na utafakari uanzie wapi katika kesho yako
Kama una ndoto za kupata mafanikio, kupata utajiri, au kuwa mwanasiasa maarufu bidii yako inatakiwa kuanzia hapa duniani.
Baada ya kifo hakuna nafasi ya kuwa mwanasiasa, wala injinia, Wala mkurugenzi, wala daktari..tumia vizuri hazina ya akili ya akili uliyonayo pamoja na hizo nguvu ambazo Mungu amekupa hasa wakati huu wa ujana.
Siku zote kesho ni ndoto za Mr. Abunuasi yeye anaamini katika kesho lakini mwanadamu mwenye malengo na bidii huanza na siku iliyokuchwa mbele yake.
Usikubali ifie moyoni mipango ya kazi na mafanikio uliyonayo. Anza kuishi, kwa sababu tunaishi mara moja. Kama ulikuwa huwezi ni vyema ujifunze kuishi kuanzia sasa.
Mhubiri mwenye hekima anasema.."Maana mwanadamu naye hajui wakati wake; kama samaki wanaokamatwa katika nyavu mbaya, na mfano wa ndege wanasao mtegoni, kadhalika mwanadamu hunaswa katika wakati mbaya unapowaangukia kwa ghafula." Mhubiri 9:12
Ikiwa kesho yetu ni giza. Unapata wapi nguvu na unajasiri wa kusema nitafanya mwakani, au miaka miwili ijayo, dunia hii inahitaji watu wenye kiu ya kufanikiwa mfano wa sungura pori kwa mbio zake.
Je! wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme, hatasimama mbele ya wasio na cheo. Mithali 22:29
Kumbe kupanga ni kuchagua, upitie changamoto za kila siku na kuweka bidii ili uishi kama mfalme au ukajutie kaburini
Basi amua leo
1. Unautaka wokovu?Utafute wokovu kwa nguvu zako ukiwa hai, kwa sababu hakuna nafasi nyingine baada ya kifo. Vinginevyo utakuwa umechagua kwenda motoni
2. Pambania maono yako kwa ujasiri, na kuweka bidii ya kuchangamana na wale ambao wana msaada katika njia za maono na ndoto zako
3. Tembea katika misingi na njia zenye kuleta ndoto timilivu maisha mwako. Achana Mambo yenye kupoteza muda na upuuzi ndani yake
Usisahau Mhubiri (Suleman) katika neno hili
"Mkumbuke muumba wako siku za ujana wako, kabla hazijaja siku zilizo mbaya..." Mhubiri 12:1
Zilizo mbaya ni zipi?
-Huenda ni kifo
-Pengine uzeeni ukiwa maskini sana usiyejiweza
-Labda ulipata ajali mbaya na hukufanikiwa kufanya lolote wakati ulipokuwa na nafasi ya kufanya hivyo
Inaelezwa kuna wasomi wengi wamezikwa na maarifa yao kaburini, akili zao na mipango ambayo huenda ingeacha urithi wa milele kwenye familia zao, nchi zao au ulimwengu.
Kwa sababu walifikiri kufanya kesho, au pengine uvivu uliwagharimu, au walikosa ujasiri na uthubutu wakazama na majuto yao kaburini.
Imeandaliwa;
Student wa Bible Class
Kapinga Jr
0718143834, kapingaemanuel@gmail.com
.jpeg)
Chakula bora cha roho.. Amen
ReplyDelete