SIRI ZA BIBLIA: Mengi uyaonayo duniani yapo katika uwezo wa shetani isipokuwa hili

 


MENGI UYAONAYO DUNIANI YAPO KATIKA UWEZO WA SHETANI ISIPOKUWA HILI....

Ayubu 1:12

BWANA akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa BWANA.

👉🏽 Siku moja nilikutana na mama mmoja kwenye daladala, akiwa ametoka kwenye kanisa la nabii flani. Usiku amechoka na mtoto mgongoni. Akaniambia kwa kweli nampenda sana huyu baba kwa kuwa anawaumbua mno wachawi.

👉🏽 Niliumia sana moyoni, nikasikia simanzi mno ndani yangu, bahati mbaya nilikuwa nafika ninaposhuka, nikasema tuna safari ndefu sana kuelekea wokovu. Shetani alipoomba ridhaa ya kuharibu maisha ya Ayubu Bwana alimwambia yote yapo katika uweza wake.

👉🏽 Nataka nikwambie leo, vitu vyote unavyotamani kuvipata katika maisha yako hata shetani anaweza kukupatia. Rejea alipomjaribu Yesu kule jangwani. Magari ya kifahari, nyumba, Kazi, biashara, dhahabu na fedha vyote unaweza kuvipata kwake ili ajitukuze katika ufalme wake wa giza na kuziangamiza roho za watoto wa Mungu.

👉🏽 Hata ile miujiuza mikubwa ya uponyaji uionayo kwenye makanisa mengi ya sasa, inaweza kufanyika kupitia uwezo wake. Maana ilishaandikwa;

"Ufunuo 18:3

kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake."

👉🏽 Si upako, wala miujiza, wala mali, wala fedha, wala dhahabu vyenye thamani mbele ya wokovu. Wokovu ndiyo jambo kubwa na la thamani ambalo shetani hawezi kukupa kwenye maisha yako. Ndiyo zawadi yenye thamani zaidi ambayo Mungu ataka kumpatia mwanadamu.

👉🏽 Wokovu wapatikana kwa YESU Kristo, yeye ni uzima, maana uzima wa milele wapatikana kwake, na kwake kuna uzima tele. Kristo anasema

"Yohana 14:6

Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi."

👉🏽 Mpendwa nataka uelewe kwamba tiketi ya safari ya kuelekea mbinguni yapatikana kwa Bwana YESU, hakuna shortcut. Mpokee YESU awe Bwana na mwokozi wa maisha yako. Kwa Yesu ni zaidi ya yote miujiza, fedha, mali, na utajiri.

👉🏽 Kuliko kuhadaika na mambo ya miujiza, mali na mahangaiko ya dunia, ni afadhali kukimbilia wokovu, kuupokea na kuuishi. Ile uwe miongoni mwa wale waabuduo halisi.

👉🏽 Yesu anasema tutafute kwanza ufalme wake na haki yake, mengine yote tutazidishiwa. Hakuna maana kupokea mali na miujiza ikiwa roho yako haijaokolewa na injili ya kweli.


Imeandaliwa; 

Kapinga JR 

STUDENT of BIBLE Class  

kapingaemanuel@gmail.com 

0718143834 

Comments