Sehemu ya pili
Unawezaje kuhusiana na Mungu bila Roho? Ukweli ni kwamba haiwezekani. Hatuwezi kuhusiana na Mungu kwa jinsi ya mwili bali Roho; Mungu alipoamua kumuonyesha Ezekiel maovu wafanyayo wazee wa Israel gizani wala haikuwa kwa jinsi ya mwili bali Roho, maana roho ndiyo iliyomuinua na si mwili.
"Naye akanyosha mfano wa mkono, akanishika kwa kishungi kimoja cha nywele za kichwa changu; nayo roho ikaniinua kati ya dunia na mbingu, ikanileta katika maono ya Mungu mpaka Yerusalemu, mpaka mlango wa kuingilia ua wa ndani uelekeao upande wa kaskazini; mahali palipokuwa pamewekwa sanamu ya wivu, itiayo wivu. 4 Na tazama, huo utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwapo hapo, sawasawa na maono yale niliyoyaona katika bonde." Ezekiel
Kabla ya kuondoka kwa Yesu Kristo aliahidi kuleta msaidizi atakayetuongoza kusimama sawa sawa na kusudi la Mungu. Yesu mwenye alisema;
"Nami nitamwomba Baba, naye atawapa msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele..." Yohana 14:16
"Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu ili kuwapasha habari." Yohane 16:14
Mpendwa kama ulivyomsikia YESU mwenyewe, hatuwezi kujua kusudi lake, hata habari zake kama hatuna huyu msaidizi ambaye alimleta kwetu ili tusibaki yatima.
Lakini ana masharti yake, ili umpokee huyu msaidizi ni lazma ukubali kuwa mwana wa Mungu, hakuna namna nyingine vinginevyo utakuwa unatwanga maji kwenye kinu.
"Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika wana Mungu, ndiyo wale waliaminio jina lake." Yohana 1:12
Ndugu yangu kama hujampokea YESU KRISTO na kuliamini jina lake kuwa ndiye Bwana na mwokozi wa maisha yako, basi utapoteza haki ya kuwa mwana wa Mungu. Utapoteza kibali cha kuhusiana na Mungu kwenye maisha yako kwa kuwa Mungu anahusiana na mwanadamu kwa jinsi ya roho. Mtume Paulo anasema hao wenye kuongozwa na roho wa MUNGU ndiyo wana wa MUNGU (Rumi 8:14). Hakuna namna nyingine.
Ili kuzifahamu siri za mbingu na kupokea mafunuo ya Mungu katika maisha yetu tunamuhitaji Roho Mtakatifu, kwa nguvu zetu, akili zetu, elimu yetu wala hatuwezi bali kupitia Roho Mtakatifu; "Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu." 1 Kor 2:10
Siku za leo kuna madhehebu mengi na makanisa mengi sana huchanga michango mingi na mikubwa ili kujenga makanisa makubwa na ya kifahari, lakini ndani yao BWANA hayupo wala makanisa yao hayaongozwi na roho. Je Mungu anahitaji yote hayo?
Yesu aliwahi kuwaambia wayahudi; "...livunjeni hekalu hili nami katika siku tatu nitalisimamisha." Yohana 2:19. Ajabu ni kwamba hawakumuelewa Yesu na yapo makanisa na madhehebu mengi huenda hawamwelewi Yesu mpaka sasa.
Makanisa makubwa na nyumba za ibada za gharama hazina maana kwa Mungu ikiwa waumini wa makanisa wamekufa kiroho, ikiwa Yesu hayupo ndani yao, wala hawajampokea Roho au kuongozwa naye.
Yupo mtumishi mmoja wa Mungu alisikia sauti ya BWANA ndotoni ikimwambia, majengo makubwa wajengayo na hayo makanisa hayana maana ikiwa watu wake wamekufa kiroho. Wala hayataki
Ikiwa watu wanajenga makanisa ya gharama lakini YESU hayupo kwenye maisha ya waumini, wanakuwa hawana tofauti na wale wayahudi ambao hawakumwelewa YESU juu ya habari ya ujenzi wa hekalu kwa siku tatu. Maana Yesu alizungumzia kazi ya msalaba uletao wokovu kwa watu wote.
Injili za uchumi na kutiana moyo kwenye mambo yasiyo na msingi kiroho zimepewa kipao mbele siku za leo huku roho za waamini zikiteketea ukosefu wa kweli ya Mungu.
Kesho itaendelea
Imeandaliwa;
Kapinga Jr
Student of Biblie Class
0718143834, Mbezi makabe, DSM
Email:kapingaemanuel@gmail.com
.jpeg)
Comments
Post a Comment