Mtu asikudanganye, hakuna nafasi ya pili ya kusamehewa dhambi baada kufa.

 


Yesu aliposema "Kesheni Mkiomba" hakuwa na maana tusilale kupumzisha miili yetu kila siku, bali tusilale usingizi rohoni, tukajisahau, nayo dhambi igeuke kuwa msiba kwetu wakati wa ujio wake. 


"Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu." Luka 21:36 


YESU anataka tuwe tayari, anataka uwe bize kumtafuta kila wakati hata katika shughuli zako, kazi zako, safari zako, kutembea kwako, kukaa kwako unayo nafasi ya kumtafuta Mungu. Endelea kuomba, endelea kusoma neno, endelea kuomba toba na rehema kwa Mungu kila wakati. Muda wa kuomba unao hata sasa maana tunahusiana na Mungu kwa jinsi ya Roho naye anasikia. Yupo na sisi kila mahali, kila eneo, hata tukiwa katika usafiri wa anga. Hii ndiyo ilikuwa maana ya YESU aliposema tukeshe. Tuwe macho huku rohoni, tujiandae.


Ijaze taa yako mafuta, ijae, uwe tayari kila giza linapoingia, hata kwa ghafla ili kipindi Bwana harusi atakapokuja awakute wanawali wakiwa tayari. Maana Yesu atakuja kama mwivi avamiavyo nyumba. Soma habari ya wanawali 10 (Mathayo 25:1-13)


Tendo la mwanadamu kusubiri kuombewa baada ya kifo na ikiwa anazo taarifa za ujio wa Bwana harusi ni wazi hakuna tofauti kati yake na wale wanawali watano waliokosa busara, licha ya kujua ujio wa Bwana harusi utakuwa muda wowote. 


Yapo makanisa, wapo wahubiri, yapo madhehebu yenye kuaminisha watu kwamba  mwanadamu atapewa nafasi ya pili kwa maombezi ya waumini hapa duniani na kwa sadaka zao. Maana baada ya kifo ni hukumu. 


Toba ni kati ya mwanadamu na Mungu, fanya toba uamkapo, utembeapo, ulalapo, omba, omba, omba Mungu anaijua nia yako, bidii yako, Roho atakuongoza ipasavyo. Kamwe toba haiwezi kushikiliwa/wala kuamriwa kwenye mikono ya mwanadamu bali Mungu mwenyewe. Omba, endelea kuomba maana hakuna muda. Omba bila kukoma (1 Thesa 5:17). Ijaze taa yako mafuta, ijae, kuwa tayari. 


Kuna watu wanapewa mafundisho ya matumaini, kwamba zipo dhambi nyepesi zinazosamehewa katika kanisa la pili kwa maombezi ya waumini wa kanisa la kwanza hapa duniani, kwa sala na Sadaka zao unanyakuliwa kupelekwa mbinguni. Mungu aturehemu sana.


Jiandae mpendwa, uwe tayari, usidanganyike.


KapingaJr 

0718143834 

kapingaemanuel@gmail.com

Comments

Post a Comment