Yesu mwenyewe alitufundisha na hata sasa anatufundisha kupitia andiko hili
Mathayo 6:33
Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
Kamwe haitawezekana Mungu akufikirie juu ya ufalme na utajiri wa dunia hii kabla ya ufalme wake kwanza. Maana utajiri wa Mungu kwa watu wote ni uzima wa milele utokao kwake.
Yesu alipokaribia kuwaacha wanafunzi wake yeye mwenyewe anawaagiza
"Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; 47 na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu." Luka 24:46-47
Yesu hakusema watu wake wahubiriwe habari za utajiri kwanza, maana haya yote tutazidishiwa kwa kadiri vile tunavyotii na kuenenda katika mapenzi ya Mungu.
Lakini adui amefahamu mpango mzuri wa Mungu kwa watu wake, maana katika injili upo wokovu na uzima naye amejiinulia watu ili kuweza kuliteka hata lile kundi la wateule. Na kwa sababu nyakati hizi wengi wanapigwa na uchumi naye adui ametumia eneo hilo kujinyakulia watu wake, atakaozama nao katika moto wa milele.
Kwa sababu ya tamaa za mali na utajiri wa haraka, kukosa subira katika ahadi za Mungu hata wateule nao wameiacha injili ya kweli na kukimbilia miujiza. Watu wa wamekataa kuwa kuwa waabuduo halisi, wamemkana yule Yesu aliyejidhihirisha Katika Yohana 4:23-34
Paulo anasema 👇🏾
Warumi 1:16
Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Mgiriki pia.
Ndugu yangu nataka nikwambie kwamba kama unakesha kwenye ibada za makanisa yasiyofundisha habari za wokovu ule uletao uzima ndani yako, hapo kimbia maana utaangamiza roho yako. Maana hakuna wokovu pasipo kumjua Kristo, maana ukimjua Kristo umeshinda vita yote na kumshinda yule adui.
Nyakati hizi adui amefahamu Roho ya Mungu haipendi huzuni naye ameweka mtego na makundi ya watu Elfu kwa maelfu wamenasa kwenye mitego yake, amefanikiwa. Maana watu wa leo wanafanikiwa kupokea mali na utajiri lakini hawawezi kuacha uzinzi, wala Uasherati wala, uongo, wala masengenyo na unafki.
Waamini hao wala hawana Roho wa Mungu ndani yao, wala hawaongozwi na huyo Roho nao wamepotea. Naye shetani amejibanza pembeni akiwacheka kwa maana katika habari ya uzima wamepotea. Hakuna anayeweza kuwa mwana wa Mungu bila Roho.
Andiko la Petro limetimia
"2 Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa. 3 Na kwa tamaa yao watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa;..." 2 Petro 2:2-3, ndugu yangu andiko katika Petro linasema hukumu yao ipo tayari wala haikawii. Nakusihi usiwe miongoni mwao mngoje Bwana kwa saburi huku ukiendelea kumtafuta Mungu kwa bidii. Usifuate mkumbo kama hao waliomchagua tumbo kuwa mungu wao.
Ndugu yangu kuna watumishi wengi wanatumia fursa, ujinga na umaskini wa kujipatia utajiri kwa mafundisho ya ujanja na uongo, wameipindisha kweli na wala ondeleo la dhambi na uzima wa milele si kipaombele kwao.
Roho aliyesema na Paulo anayadhihirisha mafundisho yake wazi wazi siku ya leo
"Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine wataikana imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; 2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;" 1 Timotheo 4:1
Maandiko yanatueleza kuwa Paulo alikuwa na upako kiasi kwamba hata leso na vitambaa viliwafungua watu wenye mapepo. Lakini hakuwahi kuhubiri juu ya mafundisho ya kuvuka Yordani wala mito ya upako bali ule uzima ultra wokovu kwa watu wa Mungu.
Anasema Paulo
1 Worintho 9:16-18 BHN
16 Ikiwa ninaihubiri injili, hilo si jambo la kujivunia; hilo ni jukumu nililopewa. Na, ole wangu kama sitaihubiri injili! 17 Ningekuwa nimeichagua kazi hii kwa hiari, basi, ningetazamia malipo; lakini maadamu naifanya ikiwa ni wajibu, hiyo ina maana kwamba ni jukumu nililopewa nitekeleze. 18 Mshahara wangu ni kitu gani, basi? Mshahara wangu ni fursa ya kuihubiri Habari Njema bure, bila kudai haki ninazostahili kwa kuihubiri.
Kwa Paulo Injili ni wajibu, lakini kwa watumishi wengi wa injili siku za leo kwao Injili ni eneo la kuchuma utajiri, wala hawana kiasi kwa ajili ya tamaa ya utajiri, imewalazimu kuigeuza nyeusi kuwa nyeusi kuwa nyekundu kwa ajili kujizolea sadaka kede kede.
Paulo na mitume wengi wa Bwana kama Petro, Yohana, Yakobo na kadhalika hawakutumia Injili kujitajirisha bali kuwaokoa mataifa katika dhambi na kuwafundisha njia ya uzima wa kweli yote katika Kristo.
Amka mpendwa fumbua macho yako na uruke hiyo mitego ya shetani vinginevyo utaangamia. Injili ya Bwana ni ile ya uzima, ikuokoayo katika hatari ya dhambi, na wala hakuna muda mpendwa, rudi kwa Yesu akuokoe.
Haijalishi utachelewa namna gani utajiri wa rafiki zako na ndugu zako usikutoe mwenye reli. Mngoje Bwana katika uaminifu atakupa mafanikio yako katika wakati wake ufaao. Maana ahadi za Bwana ni thabiti na kweli.
Zaburi 37:7
Utulie mbele za BWANA, Nawe umngojee kwa subira; Usihangaike juu ya afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu apangaye maovu.
Bwana Yesu akubariki sana
Kapinga Jr
0718143834
kapingaemanuel@gmail.com
DSM

Comments
Post a Comment