SIRI ZA BIBLIA: Je, utahukumiwa kwa neno au mapokeo



Shalom popote ulipo mwana wa Mungu


Sefania 1:12


Kisha itakuwa wakati ule, nitauchunguza Yerusalemu kwa taa; nami nitawaadhibu watu walioganda juu ya masira yao; wasemao katika mioyo yao, BWANA hatatenda mema, wala hatatenda mabaya.


Leo nimeamka na ujumbe huu wa BWANA, ambao Roho amesema andika, na watoto wangu wasome na kusikia kwa masikio yao.


Mpendwa nataka nikukumbushe kwamba hatutahukumiwa kwa mapokeo wala tamaduni za makanisa, wala kabila zetu mbele za BWANA Mungu wa majeshi bali neno lake. 


Taa ni nini? 


"Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu." Zaburi 119:105 


Kumbe taa ni neno la Mungu mwenyewe. Ndiyo tochi imulikayo mbele yetu kutuonyesha njia sahihi na mahali salama pakupita. 


Ndiyo maana anamwagiza nabii Sefania akisema waambie nitauchunguza Yerusalemu kwa taa maana yake atakuhumu watu wake kwa neno lake. Katika maisha yetu, Ukristo ni neno la Mungu na wala si mapokeo. 


Watazame siku za leo waliozama katika janga la udini, udhehebu, na mapokeo yaliyokosa neno la Mungu wanavyozama gizani kwa matendo yao, wameacha neno la Bwana na kufanya vile wapendavyo..wamezama gizani. 


Mpendwa ikiwa Yesu mwenyewe ndiye neno la Mungu (ufunuo 19:13), na ndani yake ndipo ilipo ile nuru ing'aayo sana, maana kwa kumpokea yeye ndipo tunapokea ile nuru ya utukufu ituwekayo salama anapokuwa ndani yetu, hapo na sisi hung'azwa kwa utukufu wake. 


"Kwa kuwa Mungu, aliyesema, nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo." 2 Kor 4:6 


> Kama bado unafungwa na mapokeo wewe upo gizani 


> Kama bado unapindisha neno la Mungu kwa kutetea maslahi ya kanisa au mchungaji hakika upo gizani 


> Kama neno la mchungaji au kiongozi wako wa kiroho lina nguvu kuliko neno la Mungu hakika unahitaji msaada. 


> Kama bado unashindania vita ya madhehebu kuliko kumtazama Kristo basi upo gizani. 


> Kama huduma yako ina nguvu na kiburi kuliko unyenyekevu mbele za Mungu, neno halisemi hivyo, umeangamia.


Anza tabia ya kupenda maandiko, ukiyachunguza kwa kina na kujifunza kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Maana pasipo Roho andiko halina tofauti na gazeti.."maana neno huua, Roho huhuisha" 2 Kor 3:6b, katika Roho ndipo tunafunuliwa Kristo halisi. 


Yesu aliyaona haya yeye mwenyewe aliwaonya mafarisayo akisema;


"Mathayo 15:6 


....basi asimheshimu baba yake au mama yake. Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu."


Siku zinakuja kila mmoja atalipia kwa kadiri ya kazi yake (Ufunuo 20:13); kazi zote zitapimwa kwa moto, nao moto utaijaribu kazi ya kila mmoja (1 kor 3:13), maana mwanga ndiyo chachu ya neno la Mungu. 


Mapokeo hayatakusaidia mpendwa, simama na Yesu, tembea katika moto wa maombi na katika neno la Kristo Roho atakufunulia siri zote za ufalme. 


Mwenye sikio na asikie neno hili Roho asemayo na kanisa.


Kapinga Jr,

0718143834

kapingaemanuel@gmail.com 

DSM

Comments

  1. Thank you Mtumishi , nmeelewa vyema juu ya kufuata neno la Mungu linataka nini na sio mapokeo ya dini, kanisa au dhehebu.

    Ila Kuna kitu kinanitatiza kidg juu ya ule mstari wa Biblia unaosem "kilichokubaliwa duniani na mbinguni kimepitishwa" Kwa maana hawa watu wa mapokeo wanadai hata Mungu anayakubali Kwa kuwa yamekubaliwa duniani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Neno ndiyo msingi wa imani yetu hakuna kingine. Umeona anachosema kwenye Sefania 1:12 kila jambo litapimwa kwa neno la Mungu

      Delete

Post a Comment